Recent Posts

PropellerAds

Saturday, April 16, 2016

Papa Francis arejea na wahamiaji Vatican

Kiongozi wa kanisa Katoliki duniani Papa Francis
amewachukua wahamiaji 12 kutoka Syria na kwenda nao
Vatican baada yake kutembelea wahamiaji katika kisiwa
cha Lesbos nchini Ugiriki.
Wahamiaji hao kutoka familia tatu wote ni Waislamu,
na miongoni mwao kuna watoto sita.
Nyumba za familia hizo zilishambuliwa kwa mabomu
wakati wa vita nchini Syria.
Vatican imesema kupitia taarifa kwamba Papa Francis
amechukua hatua hiyo kuwaonesha wahamiaji kwamba
wanakaribishwa.
Maelfu ya wahamiaji kwa sasa wamekwama katika kisiwa
cha Lesbos kufuatia mkataba wa mwezi jana kati ya
Umoja wa Ulaya na Uturuki ambao unalenga kupunguza
idadi ya wahamiaji wanaoingia Ulaya.
Baba Mtakatifu aosha miguu ya waislamu
Papa Francis: Donald Trump 'si Mkristo'
Kwa Picha: Maisha ya Papa Francis
Wahamiaji wote walioondoka na Papa walikuwa tayari
wanaishi Lesbos kabla ya mkataba huo kuanza
kutekelezwa, Vatican imesema.
Chini ya mwafaka huo baina ya EU na Uturuki,
wahamiaji wanaofika kwa njia haramu katika visiwa vya
Ugiriki kutoka Uturuki baada ya tarehe 20 Machi
watakuwa wakirejeshwa Uturuki iwapo hawatafanikiwa
kuomba hifadhi.
Kwa kila mhamiaji wa Syria anayerejeshwa Uturuki, EU
itampokea mhamiaji mwingine kutoka Syria aliyeko
nchini Uturuki.
Awali, Papa Francis aliambia wahamiaji wanaoishi katika
kambi ya wakimbizi ya Moria, baadhi wakikabiliwa na
uwezekano wa kurejeshwa Uturuki, kwamba "hamjaachwa
peke”.