Bunge la Afrika kusini litajadili hoja ya kumng'oa rais
Jacob Zuma madarakani siku ya Jumanne.
Spika wa bunge la Afrika Kusini ametoa taarifa hiyo
baada ya shinikizo kutoka kwa vyama vya upinzani
vikiongozwa na kile cha Economic Freedom Fighters
(EFF) kinachoongozwa na Julius Malema.
Spika Baleka Mbete, amesema wakati umewadia wa
kujadili wito wa kumfuta kazi rais Zuma kufuatia tuhuma
za ufisadi ubadhirifu wa mali ya umma na matumizi
mabaya ya madaraka yake.
Vyama vya upinzani vilikuwa vimemtaka ajiuzulu baada
ya kupatikana na hatia ya kutumia madaraka yake
vibaya kwa kuidhinisha ukarabati wa makazi yake licha
ya kushauriwa asifanye hivyo.
Siku ya Alhamisi, mahakama kuu ya nchi, ilisema kuwa
rais amekwenda kinyume na katiba, katika kashfa ya
mamilioni ya dola, yaliyotumiwa kukarabati nyumba yake
ya binafsi.
Upinzani uliwasilisha kesi mahakamani baada ya bwana
Zuma kupuuza uamuzi wa mwaka 2014 kuwa alinufaika
kutokana na ukarabati wa nyumba yake na kwamba
alistahili kulipa pesa zilizotumiwa.
Mahakama ilisema wizara ya fedha itatambua ni kiasi
gani cha pesa kilichotumiwa na kwamba Zuma
atatakikana kuzirejesha.
Rais Jacob Zuma alikubali uamuzi wa mahakama ya
kikatiba uliompata na hatia na akaapa kulipia ukarabati
uliofanyiwa makao hayo ya Nkandla kama ilivyoamua
mahakama.
Wananchi 400 wapimwa Arusha bure,Wagonjwa wa presha waongezeka “watu 100
wana presha”
-
Kituo cha afya cha Adn care kwa kushirikiana na serikali wamefanya vipimo
vya magonjwa mbalimbali bure kwa wananchi 400 wengi wao wakiwa ni kutoka
Arusha...
4 hours ago