Recent Posts

PropellerAds

Saturday, April 2, 2016

Obama: Trump haelewi sera za kigeni

Mgombea wa kiti cha urais wa Marekani kwa tiketi ya
chama cha Republican Donald Trump, hana ufahamu
wowote wa sera za kigeni wala maswala ya ulimwengu!
Haya ni kulingana na rais wa Marekani Barrack
Obama.
Obama ameyasema haya kufuatia matamshi ya Donald
Trump kuwa wanajeshi wa Marekani wanafaa kuondoka
Japan na Korea Kusini, na mataifa hayo yanafaa
kutengeneza zana zao za kinyuklia.
Mataifa hayo mawili pia hayakufurahishwa na matamshi
ya bwana Trump.