Recent Posts

PropellerAds

Saturday, April 30, 2016

Urusi na Marekani zalaumiana kuhusu uchokozi wa ndege

Urusi inasema kuwa ilikuwa na haki kuikabili ndege
moja ya Marekani katika bahari ya Baltic siku ya
Ijumaa.
Hatua hiyo inajiri baada ya Marekani kusema kuwa
ndege ya kijeshi ya Urusi ilizua hofu ya kiusalama
baada ya kuzunguka karibu na ndege yake.
Urusi inasema kuwa ndege hiyo ya Marekani ilikuwa
imezima kifaa chake cha kurusha ishara zake ambazo
husaidia wengine kuitambua.
Ni kisa cha pili katika bahari ya Baltic mwezi huu
ambapo Marekani imezishtumu ndege za Urusi kwa
kupaa kwa uchokozi.
''Ndege zetu zote za Urusi zinafuata sheria za
kimataifa kuhusu utumiaji wa anga'',taarifa ya wizara ya
Ulinzi nchini Urusi ilisema.
''Ndege za Marekani zina mambo mawili:Zisiruke karibu
na mpaka wetu ama ziwashe ishara ili kutambulika''.
Ndege za Marekani mara kwa mara hujaribu kupaa
karibu na anga ya Urusi bila taa zinazoonyesha ishara
taarifa hiyo ilisema.
Katika kipindi cha miezi 18 iliopita,Urusi pia
imeshtumiwa kwa kutekeleza kitendo kama hicho katika
bahari ya baltic pamoja na karibu na maji ya Uingereza.