Msikiti uliokuwa ukikarabatiwa umeporomoka nchini
Somalia na kuwaua watu 15 na kuwajeruhi wengine 40.
Kisa hicho kilitokea katika msikiti mmoja wa mjini
Mogadishu wakati wa ibada ya Ijumaa.
Hatahivyo maelezo yalitolewa siku ya Jumamosi.Mamia
ya watu walidaiwa kuwa ndani ya msikiti huo wakati
ulipoporomoka na wengine wanaaminika kuwa chini ya
vifusi vya jengo hilo la ibada.
Muhandisi mmoja aliyekuwa akiufanyia ukarabati
misikiti huo alikamatwa kwa tuhuma za
uzembe,vyombo vya habari vya eneo hilo
vimeripoti.Mvua kubwa imenyesha katika eneo hilo
katika siku chache zilizopita.
Serikali ya Somalia inadhibiti Mogadishu na miji
mingine,lakini wapiganaji wa al-Qaeda wanaoshirikiana
na kundi la wapiganaji wa al-Shabab wanatawala
maeneo mengi ya mashambani.
Zaidi ya wanajeshi 22,000 wa Umoja wa Afrika na polisi
wamepelekwa nchini humo kuilinda serikali.
Habari kubwa Magazetini Kenya leo March 3, 2025
-
Good Morning Mtu wangu wa nguvu kutoka Tanzania March 3, 2025,nakukaribisha
kutazama kile kilichoandikwa katika kurasa za mbele na za nyuma Magazetini
ke...
5 weeks ago