Rais wa Sudan Omar al-Bashir ameambia BBC kwamba
ataondoka madarakani mwaka 2020 muhula wake wa
sasa utakapomalizika.
Bw Bashir pia amekanusha tuhuma kwamba wanajeshi
wake wamekuwa wakitekeleza dhuluma kwenye vita vipya
dhidi ya wanavijiji weusi katika eneo la Darfuf,
magharibi mwa nchi hiyo.
Kiongozi huyo anatafutwa na Mahakama ya Kimataifa ya
Uhalifu wa Kivita (ICC) kwa tuhuma za kutekeleza
mauaji ya halaiki na uhalifu wa kivita.
Bw Bashir amekuwa madarakani tangu 1989. Alishinda
uchaguzi mkuu Aprili mwaka jana.
Ameambia mwandishi wa BBC Thomas Fessy kwamba
kazi yake “inachosha” na kwamba muhula wake wa
sasa utakuwa wa mwisho.
“Mwaka 2020, kutakuwa na rais mpya na nitakuwa
rais wa zamani,” amesema.
Hata hivyo, wakosoaji wake watasema tayari amewahi
kuahidi kung’atuka awali lakini baadaye akakosa
kutimiza ahadi hiyo, mwandishi wa BBC anasema.
Kijana aliyevuma kutokana na saa akutana na
Bashir
Afrika Kusini yapoteza kesi ya Bashir
A Kusini:Serikali yakana kumtorosha Bashir
Umoja wa Mataifa umesema zaidi ya watu 2.5 milioni
wamefurushwa makwao Darfur tangu 2003, zaidi ya
100,000 wakitoroka makwao mwaka huu pekee.
Rais Bashir amesema hakuna haja ya kuwa na walinda
Amani wa Umoja wa Mataifa na wafanyakazi wa kutoa
misaada eneo la Darfur.
Amekana taarifa za kutekelezwa kwa dhuluma zaidi
maeneo ya milima ya Jebel Marra ambapo wanajeshi
wa serikali walianzisha operesheni Januari.
"Madai haya yote hayana msingi, ripoti hizo zote
hazina ukweli,” amesema.
"Namtaka yeyote azuru vijiji vilivyotekwa na wanajeshi,
na wanioneshe kijiji kimoja ambacho kimeteketezwa.
"Kusema kweli, hakujakuwa na mashambulio yoyote ya
kutoka angani.”
Rais huyo amesema wote waliotoroka mapigano
walikimbilia maeneo yanayodhibitiwa na serikali na
kwamba hiyo ni ishara tosha kwamba serikali
haiwashambulii raia.
Rais Bashir pia amesema makadirio ya UN kwamba
zaidi ya watu 100,000 wametoroka makwao eneo la
Darfur tangu Januari kwa sababu ya mapigano
“yametiwa chumvi na si ya kweli”.
Ni watu wachache sana ambao wametoroka makwao na
wamekimbilia maeneo yanayodhibitiwa na wanajeshi wa
serikali au maeneo ambayo yana wanajeshi wa kulinda
amani wa UN, kikosi ambacho hujulikana kama Unamid.
Amesema wanajeshi wa UN na walinda amani wa umoja
huo hawana jukumu kubwa la kutekeleza na wanafaa
kuondoka nchini humo.
Aidha, amesema mashirika ya kutoa misaada yanayotoa
misaada kwa wakazi eneo la Darfur hawana jukumu la
kutekeleza kwa sababu hakuna uhaba wa chakula Darfur.
Bw Bashir amesema makadirio ya Umoja wa Mataifa
kwamba watu 2.5 milioni wanaishi kambini eneo la
Darfur si ya kweli na kwamba idadi ya kweli ni watu
karibu 160,000.
Bw Bashir alipata asilimia 94 ya kura kwenye uchaguzi
wa mwaka jana ambao ulisusiwa na upinzani.
RC Singida awapa tano Uhasibu
-
Mkuu wa Mkoa wa Singida Halima Dendego ameipongeza Taasisi ya Uhasibu
Tanzania (TIA) katika mpango wao wa kukuza somo la Hisabati kwa shule za
Singida ak...
8 hours ago