Rais wa Nigeria Muhammadu Buhari amesema ana wasiwasi mkubwa
kwamba karibu theluthi mbili ya majimbo 36 nchini humo hayana uwezo wa
kuwalipa waanyakazi mishahara, licha ya kupokea udhamini kutoka kwa
serikali ya shirikisho.
Rais Buhari amesema atajaribu kuwasilisha fedha zaidi lakini ameonya kwamba serikali kuu pia inakabiliwa na matatizo ya fedha.
Ni
hivi maajuzi tu ambapo maafisa katika jimbo lililopo kaskazini
mashariki mwa nchini hiyo, waligundua uhuni wa kuwalipa mishahara
wafanyakazi hewa wa serikali.
Hatua zilichukuliwa kuwasaka na
kuwaondosha wafanyakazi hao hewa kutoka orodha ya wafanyakazi wa
serikali, na mamilioni ya dola yaliokolewa.
Nigeria, ambayo ni nchi inayozalisha mafuta ya kiwango kikubwa Afrika, imeathirika pakubwa na kushuka kwa bei za mafuta