Mamilioni ya mashabiki wa
mwanamuziki maarufu wa muziki wa Soukus Papa Wemba aliyeaga dunia hapo
jana akiwa na umri wa miaka 66 wamekuwa wakituma rambirambi zao kwa
msanii huyo nguli aliyewaongoa wengi barani Afrika na kote duniani kwa
vibao vyake maarufu.
Yamkini Papa Wemba aliwatambua kuwakuza na kuwafunza mamia ya wanamuziki kote barani Afrika.Baadhi yao wamekuwa wanamuziki watajika kama vile Angelique Kidjo wamekuwa wakizungumza na idhaa ya BBC.
Angelique Kidjo
Bi Kidjo alisema kuwa amehuzunishwa sana na kifo chake Papa Wemba na kusema kuwa ni pigo kubwa kwa tasnia ya muziki hususan baada ya kuaga dunia majuzi kwa mwanamuziki wa muziki wa Punk Prince.
''Nimehuzunika sana tangu kuaga dunia kwa Prince kisha tena Papa Wemba, Sijui ni nini kinachoendelea huku.''
''Nilipokuwa nikifanya naye kazi niligundua ni mtu mkweli muoga lakini mweledi wa kazi yake.''
Mamilioni ya mashabiki wa
mwanamuziki maarufu wa muziki wa Soukus Papa Wemba aliyeaga dunia hapo
jana akiwa na umri wa miaka 66 wamekuwa wakituma rambirambi zao kwa
msanii huyo nguli aliyewaongoa wengi barani Afrika na kote duniani kwa
vibao vyake maarufu.
Yamkini Papa Wemba aliwatambua kuwakuza na kuwafunza mamia ya wanamuziki kote barani Afrika.Baadhi yao wamekuwa wanamuziki watajika kama vile Angelique Kidjo wamekuwa wakizungumza na idhaa ya BBC.
''Tulifanya naye klazi katika wimbo wa Ami Oh, uliokuwemo ndani ya albamu ya gwiji mwengine wa muziki barani Afrika Manu Dibango ''.
''Siku zote hata hivyo alikuwa amevalia nadhifu mno.''
''Alikuwa na maneno machache pia hakuwa msemaji sanaa.''
Manu Dibango ''Kwa hakika bara la Afrika na Tasnia ya Muziki kwa jumla imempoteza nyota wake mkubwa sana.
Bara la Afrika limempoteza mwana wao maarufu zaidi katika umbo la Papa Wemba.
Alikuwa ndiye sauti ya waafrika .
Sote sisi ni mayatima sasa.
Tunaomba kuwa roho yake ipokelewe na iwe na amani.
Papa Wemba atasalia kati yetu siku zote za maisha yetu.
Manu Dibango aliandika kwenye ukurasa wake wa Facebook .
Koffi Olomide Hili ni Janga kubwa kuikumba bara letu la Afrika.
Muziki wa kikongo umepatwa na msiba , kwa hakika muziki wa Congo umelipuliwa ,,,Sijui niseme nini
Nilisikia habari hizo lakini sikuziamini hadi pale afisa mmoja wa serikali ya Ivory Coast aliponiambia.
Kuanzia sasa maisha hayana sababu tena ,sote hatuna maana ,,tutakufa tu
Leo kwa rehema za mwenyezi mungu naomba amsamehe Papa Wemba na ampokee
Yeye ni mwana wa mungu
Natoa rambi rambi zangu kwa raia wote wa Congo na pia mashabiki wake wa Afrika
Hiyo ni sehemu tu ya ujumbe wa video aliyoitoa mwanamuziki Koffi Olomide na kuichapisha kwenye ukurasa wake wa Facebook .
Femi Kuti ''Nilipigwa na butwaa na kushtuka nilipoambiwa kilichompata ndugu yangu Papa Wemba nimehuzunishwa sana.
Yeye alikuwa akitamba tangu nyakati za Babangu Fela Kuti, Miriam Makeba, Hugh Masakela, Manu Dibango - wote hao ni vigogo wa tasnia hii barani Afrika waliotufungulia milango ya kutumbuiza nje ya bara la Afrika kama vile tamasha za muziki barani Ulaya.
Iwapo umewahi kutumbuiza kokote barani Ulaya ama hata Marekani bila shaka unamtambua Papa Wemba.
Bila shaka jina la Papa Wemba sio jina litakalotomea wakati wowote katika siku zijazo
Kuti aliiambia idhaa ya BBC kuwa Jina la Papa Wemba litadumu kwa miaka na mikaka.