Recent Posts

PropellerAds

Friday, April 15, 2016

Wagonjwa 400 wa kansa Uganda kupelekwa Kenya

MashineUganda imetangaza kwamba wagonjwa 400 wanaohitaji matibabu ya kansa watapelekwa Kenya baada ya mashine pekee ya kuwahudumia wagonjwa nchini humo kuharibika.
Wagonjwa hao ni kati ya jumla ya wagonjwa 17,000 wanaohitaji huduma ya tibaredio.
Waziri wa afya nchini humo Dkt Chris Baryomunsi aliambia bunge la nchi hiyo Alhamisi kwamba hospitali ya kibinafsi ya Aga Khan jijini Nairobi imejitolea kusaidia wagonjwa 400 kutoka Uganda wanaohitaji matibabu.
Gazeti la kibinafsi la Daily Monitor, likinukuu maafisa wa serikali, linasema nchini Uganda kuna visa 32,000 vya kansa.
Asilimia 55 (sawa na wagonjwa 17,600) wanahitaji huduma ya tibaredio.
Kwa mujibu wa Dkt Baryomunsi, serikali itagharimia usafiri na malazi huku hospitali ya Aga Khan nayo ikigharimia matibabu.
Mashine pekee nchini humo ilikuwa katika hospitali kuu ya Mulago ambayo ndiyo taasisi kubwa zaidi ya matibabu nchini Uganda na hushughulikia magonjwa makubwa.
Mashine ya tibaredio iliyokuwa Mulago ambayo ni aina ya Cobalt 60 hutoa miali nururishi, yaani Radioactive, kuangamiza seli za saratani katika mwili wa mgonjwa.
Ilinunuliwa mwaka wa 1995 na imekua ikiharibika mara kwa mara, licha ya kukarabatiwa.

Related Posts:

  • Sun Tzu's 31 Best Pieces Of Leadership Advice There was no greater war leader and strategist than Chinese military general Sun Tzu.  His philosophy on how to be a great leader and ensure you win in work, management, and life is summed up in these 33 pieces of advic… Read More
  • THE CAVE DWELLERS OF SOURTHEN SPAINUpon arrival at the bus station, Guadix looked like any other small Andalucían town, with whitewashed townhouses and charming, shaded plazas. But as I climbed to the top of the hill, a strange Martian-like landscape appear… Read More
  • Bussiness opportunity Check out Ways To Make Money on Google Play! https://play.google.com/store/apps/details?id=com.andromo.dev430081.app392812… Read More
  • Positive Youth Development Positive Experiences + Positive Relationships + Positive Environments = Positive Youth Development Based on the literature, the Interagency Working Group on Youth Programs, a collaboration of twelve… Read More
  • AINA 10 ZA BIASHARA (BUSINESS IDEAS) ZA KUFANYA SASA0Je, Unahitaji Kufanya Biashara Na Hujui Ni Biashara Ipi Ya Kufanya? Soma Hapa Kujua Ni Biashara Ipi Ya Kuifanya Sasa Wapo watu ambao mara nyingi hujiuliza ni biashara gani wafanye katika maisha yao ambayo itaweza kuwaingizia… Read More