Recent Posts

PropellerAds

Saturday, April 16, 2016

Mchezaji wa Newcastle United ahukumiwa na kutakiwa heri

Mchezaji nyota wa klabu ya Newcastle United ya
Uingereza amepigwa faini na hakimu na kisha akatakiwa
heri katika Ligi ya Premia.
Mshambuliaji Papiss Cisse, kutoka Senegal, aliadhibiwa
baada ya kupatikana na kosa la trafiki.
Alikuwa amepewa leseni ya kuendesha magari mwaka
mmoja nchini Uingereza lakini amekuwa akitumia leseni
hiyo kwa miaka mitatu.
Cisse, 30, anayeishi Darras Hall, Ponteland, alipewa
alama nne na akapigwa faini £547 na mahakimu
Newcastle.
Jedwali la msimamo wa ligi ya EPL
Klabu yake inakabiliwa na hatari ya kushushwa daraja
katika Ligi Kuu ya England na baada ya kumsomea
hukumu, mwenyekiti wa jopo la mahakimu Carolyn
Hyslop kisha alimwambia: "Kila la kheri kesho."
Newcastle United watakutana na Swansea City uwanjani
St James' Park Jumamosi kwenye mechi ambayo
wanahitajika kushinda kujiongezea matumaini ya
kunusurika.