Rais wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli ametengua
uteuzi wa mkuu wa mkoa wa Shinyanga kutokana na
kuwepo kwa watumishi hewa.
Bi Anna Kilango Malecela alitangaza kwenye vyombo
vya habari kuwa mkoa wake hakuwa na watumishi
hewa.
Ikulu hata hivyo ilifanya uchunguzi wake na kubaini
kuwepo kwa wafanyakazi hewa 45 katika awamu ya
kwanza.
Awamu ya pili ya uchunguzi huo bado inaendelea katika
wilaya mbili za Ushetu na Shinyanga Vijijini.
Wafanyakazi hewa 2,000 wagunduliwa Tanzania
Magufuli ataka wafanyakazi hewa wamalizwe
Akiongea Ikulu jijini Dar es Salaam, Rais Magufuli
amesema amesikitishwa na hali hiyo na kuagiza mkuu
huyo wa mkoa na Katibu Tawala wa Mkoa Abdul
Rashid Dachi kuondolewa kazini mara moja.
"Na wale wote wa Shinyanga ambao walisemekana ni
zero, hakuna mtumishi hewa, walikuwa tayari
wameshalipwa shilingi milioni 339.9, nimejiuliza sana,
na nikajiuliza sana na kwa kweli nimejiuliza sana na
kwa masikitiko makubwa, kwa nini mkuu wa mkoa
alisema hakuna mtumishi hewa?" amesema Dkt
Magufuli.
Kwa jumla, zaidi ya wafanyakazi hewa 2,000
waligunduliwa baada ya utathmini kufanywa mikoani.
Habari kubwa za Magazeti ya Tanzania leo January 11, 2024
-
Good Morning Mtu wangu wa nguvu kutoka Dar es salaam January 11,
2025,nakukaribisha kutazama kile kilichoandikwa katika kurasa za mbele na
za nyuma za Ma...
6 hours ago