Dar es Salaam. Rais John Magufuli leo
anakwenda Rwanda, ikiwa ndiyo ziara yake ya
kwanza ya nje ya nchi tangu alipoapishwa
kushika wadhifa huo, Novemba 5, mwaka jana.
Rais Magufuli alisimamisha safari za nje kwa
watumishi wa umma isipokuwa kwa kibali
maalumu kutoka kwake au Katibu Mkuu
Kiongozi ili kuokoa fedha nyingi ambazo
zinatumika katika safari hizo na kuzielekeza
katika shughuli mbalimbali za maendeleo.
Tangu kuapishwa kwake, Rais Magufuli
amefanya safari za ndani pekee katika mikoa ya
Dar es Salaam, Dodoma, Arusha, Mwanza na
Geita.
Ziara hiyo ya siku mbili nchini Rwanda itaanza
kwa uzinduzi wa kituo kimoja cha ukaguzi
katika mpaka wa Rusumo unaounganisha nchi
hizo kisha kufanya mazungumzo na Rais wa
Rwanda, Paul Kagame.
Kwa mujibu wa taarifa ya kituo cha habari cha
KT Press cha Rwanda, siku ya pili Rais Magufuli
ataungana na wananchi wengine wa Rwanda
katika kumbukumbu ya maadhimisho ya 22 ya
mauaji ya kimbari yaliyotokea mwaka 1994.
Rais Magufuli ambaye ameambatana na mkewe
Janeth, ataweka shada la maua kwenye
makaburi hayo na kuwasha mwenge maalumu.
Baadaye Rais ataungana na Wanyarwanda
katika matembezi maalumu, kabla ya kwenda
kwenye mkesha utakaofanyika kwenye Uwanja
wa Amahoro, Kigali.
Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje, Afrika
Mashariki, Kikanda na Kimataifa, Mindi Kasiga
alisema akiwa Rusumo, Dk Magufuli atafungua
kituo cha biashara ya pamoja “one stop border
post’.
Umuhimu wa ziara
Ziara hiyo inatarajiwa kuimarisha uhusiano wa
kibiashara baina ya mataifa haya.
Bandari ya Dar es Salaam ni muhimu kwa
uchumi wa Rwanda kwa sababu asilimia 70 ya
mizigo inayotumia usafiri wa majini, inapitia
Tanzania.
RC Singida awapa tano Uhasibu
-
Mkuu wa Mkoa wa Singida Halima Dendego ameipongeza Taasisi ya Uhasibu
Tanzania (TIA) katika mpango wao wa kukuza somo la Hisabati kwa shule za
Singida ak...
1 hour ago