Mgombea urais wa chama cha Republican nchini
Marekani Ted Cruz ameshinda mchujo wa chama hicho
katika jimbo la Wisconsin, hilo likiwa pigo kubwa kwa
Donald Trump.
Katika chama cha Democratic, Bernie Sanders alipata
ushindi mkubwa dhidi ya Hillary Clinton anayeongoza
kwa wajumbe kwa sasa.
Bw Trump anaongoza kwa wajumbe na katika kura za
maoni chama cha Republican, lakini kuna wasiwasi
kwamba huenda akashindwa kupata wajumbe wa
kumuwezesha kuidhinishwa moja kwa moja kuwa
mgombea.
Wapinzani wa Bw Trump wanatumai kwamba hilo
likifanyika basi wanaweza kubadilisha mambo katika
mkutano mkuu wa chama hicho wa kuidhinisha
wagombea mwezi Julai.
Katika mkutano huo, iwapo hakuna mgombea
atakayepata zaidi ya nusu ya wajumbe, ni viongozi wa
chama ambao watakuwa na usemi katika kuamua
mgombea.
“Leo ni siku muhimu sana, inatoa ujumbe kwa watu wa
Marekani,” Bw Cruz amewaambia wafuasi wa chama
hicho Milwaukee.
“Tunashinda kwa sababu tunaunganisha chama cha
Republican.”
Trump ayumbayumba kuhusu utoaji mimba
Trump aahidi kuvunja mkataba wa nyuklia
Bw Cruz huenda asipate wajumbe wa kutosha
kumuwezesha kushinda uteuzi moja kwa moja, lakini
viongozi wa chama cha Republican wanamuunga mkono
katika juhudi za kumzima Bw Trump.
Bw Trump kwa upande wake amesema kwamba ana
matumaini kwamba atafanikiwa licha ya kushindwa
Wisconsin na akamshambulia mpinzani wake.
"Ted Cruz ni mbaya kushinda kikaragozi, yeye ni kama
kirusi, anatumiwa na viongozi wa chama kutupokonya
uteuzi,” maafisa wa kampeni wa Bw Trump wamesema
kupitia taarifa.
Viongozi wa chama wana wasiwasi kwamba Bw Trump
hatakuwa na nguvu sana katika kukabiliana na mgombea
wa Democratic uchaguzini iwapo ataidhinishwa na pia
kwamba anaweza kuathiri wagombea ubunge wa
Republican uchaguzini.
Kura za maoni zinaonesha hapendwi na wanawake, watu
wa Hispania na vijana.
Katika upande wa Democratic, ushindi wa Sanders
jimbo la Wisconsin umemuongezea nguvu kabla ya
mchujo muhimu New York na Pennsylvania.
Seneta huyo wa Vermont, akiwahutubia wafuasi wake
Wyoming, amesisitiza kwamba kampeni yake inaendelea
kushika kasi na kwamba atabadilisha mambo.
"Mabadiliko kamili huwa hayafanyiki kutoka juu kwenda
chini, huwa yanatoka chini kwenda juu,” amesema.
Bi Clinton yuko mbele sana kwa wajumbe na wadadisi
wengi wa kisiasa wanasema ana uwezekano mkubwa wa
kushinda uteuzi wa chama cha Democratic licha ya
kushindwa majimbo kadha karibuni.
Ingawa Bw Trump alishindwa mchujo huo wa Jumanne
Wisconsin, bado ana muda wa kujikwamua.
Mshirikishe mwenzako Una
Dully Sykes afunguka kuhusu kuchelewa kuingia kwenye ndoa mpaka hivi sasa
-
Mkali na Mkongwe kwenye Game, Dully Sykes amefunguka na AyoTVENT kuhusu
Kuchelewa kuingia kwenye ndoa mpaka leo hii akiwa na miaka zaidi ya 40
ikiwa bado...
9 hours ago