Mtu mmoja ameuawa baada ya ndege moja kuangukia
gari alimokuwa kwenye barabara kuu ya California
Marekani.
Walioshuhudia wanasema kuwa ndege hiyo ilionekana
kama iliyokuwa na matatizo ya injini na ikalazimika
kutua kwa dharura kwenye barabara ya Interstate 15
freeway California.
Rubani wa ndege hiyo Dennis Hogge hata hivyo
alishindwa kuidhibiti na ikateleza na kuigonga gari
lililokuwa na abiria wanne lililokuwa limeegeshwa kando
ya barabara hiyo ilidereva azungumze kwa simu.
Mmoja aliaga dunia papo hapo huku wengine watatu
wakikimbizwa hospitalini katika hali mahututi.
Antoinette Isbelle, 38, kutoka San Diego alikuwa
ameketi nyuma katika gari hilo lililogongwa.
Yamkini hii sio mara ya kwanza kwa ndege hiyo kutua
kwenye barabra hiyo ya San Diego.
Mwaka wa 2000 mmiliki wa kwanza wa ndege hiyo
vilevile alipatwa na hitilafu ya kimitambo na akalazimika
kutua ndege hiyo hiyo chapa Lancair IV, kwenye
barabara hiyo hiyo.
Hata hivyo wakati huo tukio hilo halikusababisha maafa
wala uharibifu wa ndege hiyo.
Ihalula wakabidhiwa gari ya wagonjwa,serikali yazidi kupigilia msumari
“Marufuku mgonjwa kulipia ni bure”
-
Watumishi wa Afya Halmashauri ya Mji wa Njombe wametakiwa kutowatoza fedha
wagonjwa kwa ajili ya kulipia gari la kubebea wagonjwa kwani tayari
Serikali i...
3 hours ago