Makamu wa Rais wa Kenya William Ruto atafahamu leo
iwapo kesi inayomkabili katika Mahakama ya Kimataifa
ya Uhalifu (ICC) itatupiliwa mbali.
Mwanahabari Joshua arap Sang, aliyeshtakiwa pamoja
na Bw Ruto, pia atafahamu leo iwapo ana kesi ya
kujibu.
Bw Ruto anakabiliwa na mashtaka ya mauaji,
kuhamisha watu kwa lazima na mateso yaliyotekelezwa
wakati wa vita vya baada ya uchaguzi mkuu wa mwaka
2007.
Amekana mashtaka hayo na mawakili wake wanataka
kesi hiyo itupiliwe mbali kutokana na ukosefu wa
ushahidi.
Watu takriban 1,200 waliuawa wakati wa mapigano
hayo.
Upande wa mashtaka umekabiliwa na changamoto kadha
kwenye kesi hiyo dhidi yake.
Mwezi Februari, majaji katika mahakama hiyo waliizuia
afisi ya mwendesha mashtaka kutumia ushahidi wa
mashahidi ambao tayari wamejiondoa.
Mashahidi kadha muhimu walibadilisha taarifa zao za
ushahidi, jambo ambalo waendesha mashtaka wanasema
lilitokana na vitisho na kuhongwa.
Mawakili wa Bw Ruto wanasema anafaa kuondolewa kesi
hiyo kwa sababu mashahidi wengi wa upande wa
mashtaka wamejiondoa au wakabadilisha taarifa zao asili
za ushahidi.
Ruto ashinda rufaa mahakama ya ICC
Mashahidi wa Ruto katika ICC
Bensouda:Sikabiliwi na shinikizo zozote
Mwendesha mashtaka mkuu wa ICC Fatou Bensouda
amekiri kwamba kujiondoa kwa mashahidi kumeathiri kesi
dhidi ya naibu huyo wa rais lakini anasisitiza kwamba
bado kuna ushahidi wa kutosha wa kuendelea na kesi
hiyo.
Msemaji mmoja wa ICC ameambia mwandishi wa BBC
Anna Holligan mjini The Hague kwamba kuna mambo
kadha ambayo yanaweza kutokea.
Majaji wanaweza kuondoa mashtaka yote dhidi ya Bw
Ruto, wanaweza kuutaka upande wa mashtaka ubadilishe
mashtaka au wanaweza kukataa tetesi za upande wa
mshtakiwa na kuamua kesi iendelee.
Mwaka 2014, mwendesha mashtaka aliondoa mashtaka
sawa dhidi ya Rais Uhuru Kenyatta akisema mashahidi
walikuwa wametishiwa na kubadilisha ushahidi wao.
Hatima ya kesi hiyo sasa inaonekana kutegemea iwapo
mwendesha mashtaka alithibitisha kwamba ana ushahidi
wa kutosha wa kupinga msimamo wa upande wa
mshtakiwa kwamba hana kesi ya kujibu.
Suala la kutumiwa kwa ushahidi wa mashahidi
waliojiondoa huongozwa na Kanuni 68 ya Mkataba wa
Roma, uliounda mahakama ya ICC.
Mawakili wa William Ruto walisema haikuwa haki kwa
sheria hiyo kutumiwa kwenye kesi dhidi yake kwani
mabadiliko ya kuruhusu kutumiwa kwa ushahidi wa
mashahidi waliojiondoa yalifanywa baada ya kesi dhidi
yake na mwanahabari Joshua arap Sang kuanza.
Jaji Judge Piotr Hofmanski aliamua kwamba ushahidi wa
mashahidi waliojiondoa ulitumiwa bila kuwapa mawakili
wa washtakiwa fursa ya kuwahoji mashahidi hao.
Alisema haingekuwa haki kwa ushahidi huo kutumiwa
dhidi ya washtakiwa.
Bw Sang, anadaiwa kutumia vipindi vyake vya redio
kupanga mashambulio baada ya uchaguzi.
Baada ya majaji kuamua ushahidi wa mashahidi
waliojiondoa haufai kutumiwa, Bw Sang alisema hiyo
ilikuwa „hatua moja kuelekea kwa uhuru wetu”.
Bw Ruto na Bw Kenyatta walikuwa kwenye mirengo
pinzani wakati wa uchaguzi wa 2007 lakini waliunda
muungano wa kisiasa na wakashinda uchaguzi mkuu wa
2013.
Habari kubwa Magazetini Kenya leo November 24, 2024
-
Good Morning Mtu wangu wa nguvu kutoka Tanzania November 24,
2024,nakukaribisha kutazama kile kilichoandikwa katika kurasa za mbele na
za nyuma Magazetin...
56 minutes ago