Recent Posts

PropellerAds

Thursday, June 9, 2016

Kwanini ndoa za sasa hazidumu ?

Imezoeleka kwamba ndoa za kikatoliki zikifungwa zimefungwa pamoja na sharti hilo ,viwango vya ndoa zinazovunjika zinaendelea kuongezeka na kufuatia hali hiyo,kanisa katoliki limeamua kuanzisha tuzo maalumu kwa wandoa wakongwe zaidi kwa mwaka huu katika kanisa hilo.
Kanisa Katoliki jimbo kuu la Dar es salaam wameandaa kliniki ya ndoa ili kuweza kuwapa fursa wanandoa kuimarisha ndoa zao kiimani,Padre Novatus Mbaula ambaye ni mkurugenzi wa ndoa na familia anaeleza lengo la kliniki hii ni kuwapa nafasi wanandoa wa katika makundi mbalimbali kukaa pamoja kupata neno la Mungu na kuweza kuongea juu changamoto zao mbalimbali kuongea kuhusu maisha yao ya ndoa.
Ni nafasi ambayo wanandoa ambao wana uzoefu mkubwa katika ndoa wanaweza kuwafaidisha wanandoa wachanga lakini pia changamoto katika ulimwengu wetu wa sasa changamoto bado ni zilezile.
 

Miongoni mwa watu waliohudhuria kliniki hii ni wanandoa wenye ndoa yenye miaka 61,brigedia Generali mstaafu Francis Mbena,mwenye umri a miaka 86 alifunga ndoa akiwa na miaka 25 ,mwaka 1965 Juni,anasema wao zamani walikua wanafuata mtu na familia gani na ina vigezo gani?
Walikua wanaangalia tabia kama msichana hana tabia nzuri huoi huko; kama familia ina watu walevi uwaendei na unatafuta familia yenye watoto wenye tabia nzuri ili na wewe uweze kupata watoto wenye tabia nzuri.
Wakati mke wake ambaye ni Maura Stephen Mbena ambaye anasema asili yake ni Nyoni,yeye anasema ukiweza kumvumilia mwezako na ukamsamehe basi unaishi tu maana kukwaruzana kupo hakuishi na kikubwa ni kuvumilia.
Na katika mila na desturi za kabila yake ya wangoni, msichana kabla hajaolewa anaanapewa maneno na wazee ambao wazazi wako wamewaamini wanakupa msafara wote wa maisha ya ndoa,kwamba unapokwenda kuna matatizo pengine wakwe zao hawatakupenda au hautafanya vizuri kule na wanakupa muelekeo wa maisha ukavumilie na ukafanye hivi hivi lakini kikubwa sana ni sala.
Ndoa ni maisha yenye tafsiri nyingi,Bwana na bi.Alphonce Hurick walioko kwenye kipindi cha mwaka mmoja wa ndoa,wao wanaona maisha ya ndoa ni maisha yenye furaha,amani na upendo na ni maisha tofauti kabisa wakati kila mmoja akiishi peke yake peke yake,kwani hata kama una msongo wa mawazo kama ndoa yako ina furaha basi hayo matatizo yanakuwa hayapo kama ndoa yako ina upendo.
Bi.Kigadie ambaye yuko kwenye ndoa kwa miaka 46 na miezi mitano anaeleza jinsi walivyoingia kwenye ndoa na jinsi vijana wanavyoingia kwenye ndoa katika miaka ya sasa.
Anasema wengi hawakupata mafunzo ya kujua uchumba ni nini maana mapema mno wanageuza uchumba kuwa mme na mke kabla hawajapata sakramenti ya ndoa,sasa hilo ni tatizo ambalo wanajikuta wamepata ujauzito sasa ndoa inakuwa ya shuruti unaweza kuwa hata bwana alikuwa hana nia ya ndoa zaidi ya tamaa za kimwili na kimaisha.

Related Posts:

  • The Sale of Joseph and the Son of God Before we retell the story of Joseph and the spectacular sin of his brothers and its global purpose in the glory of Jesus Christ, let’s back up to Genesis 12. God has chosen Abram from all the peoples of the worl… Read More
  • Train Up a child Moms and dads, do you feel like your children’s salvation is up to you? I would never have said that, but when my kids were little, I kind of did. I thought that if I fulfilled Proverbs 22:6, they would automatically… Read More
  • Listen and Watch Closely Kings 18:1: “After a long time, in the third year, the word of the LORD came to Elijah: “Go and present yourself to Ahab, and I will send rain on the land.” According to a couple New Testament passages, this “After a long … Read More
  • Live to make Christ look magnificent. God’s Goal: Glory Oh, how I remember the tumultuous and wonderful days between 1968 and 1971, when my world was being destroyed and rebuilt by an understanding of the overarching, sovereign purposes of God to be glorified i… Read More
  • 5 Things I Learned in Church Planting By  Ron Edmondson I’ve planted two churches. In each plant, God overwhelmed us continually with what He did among us. I feel humbled and blessed to be a part of such healthy environments God uses to reach people with … Read More