Recent Posts

PropellerAds

Saturday, June 25, 2016

Uskochi yakutana kujadili hatma yake

Waziri wa maswala ya Uskochi bi Nicola Sturgeon, anakutana na baraza lake la mawaziri huko Edinburgh kujadili hatma ya Uskochi baada ya matokeo ya kura ya maoni kubaini ushindi wa kambi iliyotaka Uingereza ijitoe kutoka kwa muungano wa Ulaya.
Bi Nicola amesema anataka kuhakikisha kuwa Uskochi hailazimishwi kutoka EU kwani wao walipiga kura ya kutaka kubaki ndani ya EU.
Sasa anasema anataka kuwe na mchakato wa kuandaa kura ya maoni ya iwapo Uscochi itaitenge kutoka kwa Umoja wa Uingereza UK.
Bi Sturgeon anasema anataka hima kuweka mfumo huo kabla ya Uingereza kukamilisha hatua yake ya kujibandua kutoka EU.
Mbali na kutaka kujumuishwa moja kwa moja kwenye maamuzi yatakayochukuliwa , pia amesema mawaziri wa uskochi watawasiliana moja kwa moja na mawaziri wa nchi 27 wanachama wa EU kuhusiana na nia yao ya kutaka kusalia EU.

Related Posts:

  • Somalia yazuia raia wake kwenda Sudan Somalia imewaambia raia wake kuwa hawaruhusiwi kusafiri kwenda nchini Sudan, ambacho ni kituo maarufu kwa wahamiaji wanaosafiri kwenda Ulaya kinyume na sheria. Afisa mkuu wa uhamiaji Abdullahi Gafow, alisema kuwa wasomal… Read More
  • Google yashtakiwa kwa sababu ya android Muungano wa Ulaya EU umeifungulia rasmi mashtaka ya kujihusisha na vitendo vinavyozuia ushindani wa kibiashara kampuni ya kuhusiana na jinsi kampuni hiyo ya teknolojia inavyotangaza mfumo endeshi wa simu wa android. Kami… Read More
  • Mahakama yatupa 'sheria ya matusi' mtandaoni Kenya Mahakama Kuu jijini Nairobi imeamua kwamba Kifungu cha Sheria ambacho kimekuwa kikitumiwa kuwafungulia mashtaka watu kuhusiana na ujumbe kwenye simu na mitandao ya kijamii Kenya ni haramu. Jaji wa Mumbi Ngugi alisema kif… Read More
  • Trump na Clinton washinda New York Zaidi ya nusu ya kura zilizohesabiwa katika uchaguzi wa awali wa urais nchini marekani katika mji wa New york,zinaonesha kwamba Donald Trump na Hillary Clinton wamepata ushindi mkubwa Zaidi ndani ya vyama vyote viwili. H… Read More
  • Mwanafunzi mweusi mwislamu achaguliwa UK Mwanafunzi ambaye awali alikataa kulishtumu kundi la wapiganaji wa Islamic State amechaguliwa kuwa rais wa muungano wa kitaifa wa wanafunzi nchini Uingereza. Mali Bouattia,ambaye ataanza kuhudumu kuanzia mwezi Septemba pi… Read More