
Meya wa demokrasia ya Philadelphia,Jim Kenney alisema kodi hiyo itatumika kwenye maendeleo ya elimu na maeneo ya kupumzikia. Wakili wa afya wanasema vinywaji vyenye sukari vinasababisha watu kuongezeka uzito kupita kiasi na ugonjwa wa kisukari. Kodi hiyo imekosolewa vikali na wananchi wenye hali ya chini .Philadelphia ni mji wa pili baada ya mji wa Berkeley uliopo California kufanikiwa kuanzisha kutoza kodi ya aina hii.