Recent Posts

PropellerAds

Saturday, June 4, 2016

Paris yakumbwa na Mafuriko


Mto Seine ulioko mjini Paris, Ufaransa, umejaa na kufikia kima cha juu zaidi kuwahi kutokea kwa zaidi ya miaka 30 iliyopita.
Maji yamefurika hadi kwenye barabara na kulazimisha makavazi kadhaa na maeneo ya makaburi kufungwa.
Waziri wa Mazingira, Segolene Royale, amewaonya watu kukaa katika hali ya tahadhari wakati huu ambapo Mto Seine unazidi kupanda.
Amesema kuwa ingawa kima cha maji katikati mwa jiji la Paris kinazidi kupunguka lakini kutoweka kwa maji kutafichua madhara mengi zaidi.

Katika eneo la makavazi la Louvre, wafanyakazi wamekuwa waking'ang'ana kuokoa vifaa mbalimbali vya zamani kuhakikisha kuwa haviharibiwi na maji.
Wamekuwa wakishughulikia zaidi ya vitu 250,000 vya zamani.
Inakisiwa kuwa karibu watu 15 wamefariki kutokana na mafuriko katika mataifa manne ya Ulaya, wengi wao wakiwa kutoka Ujerumani.