Recent Posts

PropellerAds

Tuesday, June 21, 2016

Korea Kusini kurejesha vyoo vya kale

Mamlaka katika mji mkuu wa Korea Kusini, Seoul, imebadili sera zake kuhusu vyoo vya umma.
Utafiti uliofanywa ulibaini kuwa robo ya watu weote waliohojiwa walitaka kuwepo vyoo vya kale vyenye shimo badala vya kisasa.
Vyoo vya kale nchini korea kusini vilikuwa vya kuchuchumaa
Lakini serikali iliamua kuwa wakati nchi hiyo ilipounuka na kuwa tajiri, ilikuwa bora kujenga vyoo vya kisasa.
Mamlaka ya mji wa Seoul iliwahoji watu 3,137 na kugundua kuwa, karibu robo ya watu hao wanataka kurejeshwa vyoo vya kale.
Watu hao hasa wanawake wasema kuwa vyoo vya kisasa havizingatii usafi kwa sababu vinahitaji mtu kukaa kwa kiti.