Recent Posts

PropellerAds

Wednesday, June 22, 2016

Moise Katumbi ahukumiwa miaka 3 jela


Mgombea urais wa upinzani nchini Jamhuri ya Demokrasi ya Congo Moise Katumbi, amehukumiwa kifungo cha miaka 3 jela kwa kununua nyumba kinyume cha sheria kwenye mji ulio mashariki mwa nchi wa Lubumbashi.
Pia alipigwa faini ya dola milioni 6.
Katumbi hakuwa mahakamani wakati wa kutolewa kwa hukumu hiyo, baada ya kusafiri kwenda afrika kusini kupata matibabu siku moja baada ya serikali kutangaza waranti wa kukamatwa kwake kwa mashtaka tofauti.

Analaumiwa kwa kuwaajiri mamluki wa kigeni ili kipanga njama dhidi ya serikali.
Katumbi amekosoa hukumu hiyo, akisema kuwa ni jaribio la kutaka kuchelewesha kampeni yake ya kutaka kumrithi Rais Joseph Kabila mwezi Novemba.

Related Posts:

  • Dadake Prince ataka kurithishwa mali Nyota wa muziki wa Pop Prince hakuwacha wasia ,dadaake amefichua katika stakhabadhi za mahakama. Nakala zilizowasilishwa katika mahakama ya jimbo la Minnesota zinaonyesha,Tyka Nelson ametoa ombi la mtu atakayesimamia mali… Read More
  • Anonymous wavamia mtandao wa wizara Kenya   Kundi la wadukuzi wa mitandaoni la Anonymous limeshambulia tovuti ya wizara ya mambo ya nje ya Kenya na kuiba data muhimu, tovuti moja ya usalama mtandaoni imeripoti. Shambulio hilo lilitekelezwa chini ya opereshe… Read More
  • Facebook yapata faida kubwa Facebook imeripoti ongezeko la faida kwa asilimia 195 katika robo ya kwanza ya mwaka huku kampuni hiyo ikiendelea kupata mapato ya matangazo mapya. IIiripoti mapato ya dola bilioni 1.5 katika kipindi cha kati ya mwezi Ja… Read More
  • Mwili wa Papa Wemba wawasili DRC Mamia ya watu wamekongamana nje ya uwanja wa ndege wa Kinshasa kuupokea mwili wa mwanamuziki Papa Wemba uliowasili nchini humo kutoka Abidjan Mwanamuziki huyo ambaye ametajwa kuwa mmoja ya waanzilishi wa muziki wa kizazi… Read More
  • Magazeti ya Tanzania April 28 2016… Read More