
Mamlaka ya mji mmoja nchini Japan,
imeanza harakati ya kuwasaidia wanawake kugharimia malipo ya kuhifadhi
mayai yao ya uzazi- kama hatua moja ya kujaribu kuimarisha viwango vya
uzazi nchini humo.
Mji wa Urayasu, viunga vya jiji kuu Tokyo,
umetenga dola laki nane u nusu kwa majaribio hayo ya kuhifadhi mayai ya
uzazi, inayoaminika kuwa mradi wa kwanza kabisa wa aina yake duniani.Wanasayansi katika hospitali iliyokabidhiwa majukumu hayo, wanasema kwamba, wanaimani kuwa uhifadhi ya mayai hayo ya uzazi itawasaidia wanawake kujifungua watoto wakiwa wamejiandaa ipasavyo, na kuongeza muda ambao watakuwa na watoto wao.
