Mahakama moja huko Qatar imempata na hatia mwanamke raia wa Uholanzi kwa kushiriki ngono nje ya ndoa.
Alizuiwa mnamo mwezi Machi baada ya kuwaambia maafisa wa polisi kwamba alibakwa.
Mwanamke
huyo amepigwa faini ya dola mia nane na kifungo cha mwaka mmoja japo
hatatumikia jela. Kwa mujibu wa mawakili wake, mama huyo alikua
amekwenda kwenye hoteli moja ya burudani mjini Doha.
Wakati
aliporejea mezani alipokua akikunywa kinywaji chake na kuanza kusinzia,
hapo akafahamu kinywaji hicho kiliwekwa kemikali fulani.
Alipopata
fahamu alijipata akiwa ndani ya makaazi ya mtu asiyemhafamu na alikuwa
amebakwa. Msemaji wa ubalozi wa Uholanzi mjini Doha ameiambia BBC kwamba
mwanamke huyo ameachiwa huru kutoka korokoroni na anatarajiwa
kurejeshwa nyumbani.
Taarifa zaidi zinasema kwamba, mwanamme aliyepatikana na hatia ya kufanya mapenzi na mwanamama huyo amehukumiwa viboko 140.
chini Qatar ni hatia kubwa kunywa pombe au kupatikana ukiwa mlevi
hadharani. Hata hivyo kuna baadhi ya hoteli za kitalii ambapo wateja
hukubaliwa mvinyo.
Kufanya mapenzi nje ya ndoa pia ni hatia katika
nchi hiyo. Hapo mwaka wa 2013, mwanammke raia wa Norway alihukumia
miezi 16 gerezani katika nchi jirani ya Umoja wa Falme za kiarabu, baada
ya kupatikana na hatia ya kufanya mapenzi nje ya ndoa, na kuwa mlevi
hadharani.
Alipokamatwa aliwaambia polisi alikua amebakwa. Alipewa msamaha na kurejeshwa nyumbani.
Kesi
hii ya mwanamke raia wa Uholanzi inazua wasi wasi jinsi mamlaka za
Qatar zitakavyowashughulikia maelfu ya watalii wa kigeni kutoka
magharibi ambao watazuru nchi hiyo kwa fainali za kombe la dunia mwaka
2022.
Wengi wa watalii hawalewi kuhusu baadhi ya sheria hizi.
Tanzania mwenyeji mkutano 63 wa baraza la Kimataifa la viwanja vya ndege
Afrika
-
Tanzania imeteuliwa kuwa mwenyeji wa Mkutano wa 73 wa Baraza la Kimataifa
la Viwanja vya Ndege (Airports Council Interantional-ACI) kwa Kanda ya
Afrika,h...
31 minutes ago