Korea Kusini inasema kuwa majirani
zao Korea Kaskazini kwa mara nyingine tena, wameifanyia majaribio
makombora yake mawili, hatua ya wazi ya kuonesha kukiuka hatua Umoja wa
mataifa kuiwekea taifa hilo vikwazo vya kiuchumi. Taarifa zasema kombora
la kwanza halikufanikiwa huku la pili likisafiri umbali wa kilomita mia
nne.
Msemaji wa Waziri wa Umoja wa taifa wa Korea Kusini Joeng Joon-hee amesema majaribio hayo ni kukiuka vikwazo."Ulipuaji huo makombora kwa kutumia Teknolojia ya angani unakiuka maazimio ya Umoja wa mataifa. NIa ni uchokozi dhidi yetu. Tunashauri ni vyema kwa Korea Kaskazini kuzidisha nguvu katika kuimarisha amani katika eneo la rasi ya Korea na kwa maisha ya watu wake ambayo Korea kaskazini imekuwa ikisititiza kila wakati." Amesema
Naye waziri mkuu wa Japan Shinzo Abe amelaani hatua hiyo Korea ya Kaskazini.
"Leo kumelipuliwa makombora kwa kutumia teknolojia ya angani iliyotumika zamani huu ni ukiukwaji wa wazi wa azimio la Baraza la Usalama la Umoja wa mataifa. hatutarusu na tutaandaa azimio la kupinga hatua hiyo," amesema Waziri Mkuu huyo