Maafisa wa kibalozi jijini New York
wanasema kuwa hiyo kesho Umoja wa Mataifa utaomba rasmi Serikali ya
Syria kuruhusu kudondosha vyakula na madawa katika maeneo wanakoishi
wananchi walio katika hatari ya kufa kutokana na ukosefu wa chakula.
Lakini
mwandishi wa BBC katika Umoja wa Mataifa anasema kuwa dalili za awali
kutoka kwa Serikali ya Syria ni kuwa huenda idhini hiyo isitolewe.Kati ya maeneo 17 yanayokabiliwa na vita Serikali ya Rais Bashar Al Assad imetoa idhini kwa maeneo 12 pekee na idhini nusu kwa maeneo matatu.
Uingereza ilisema idhini hiyo imetolewa kama imechelewa na kwa kiasi kidogo mno. Ufaransa ilitaja hatua hiyo kama tone kwenye Bahari.