kundi la wanamgambo nchini Somalia,
al-Shabab, wanasema wamewaua watu watatu kwa kuwapiga risasi na
kumchinja shingo mwingine, baada ya kupatikana na hatia ya kuwa majasusi
wa mashirika ya ujasusi ya Kenya na Marekani.
Mauaji hayo yalitekelezwa mbele ya umati wa watu katika mkoa wa Bakool.
Kulingana na taarifa ya radio ya al-Shabaab,
mwanamume mmoja aliyeuawa ni Mohamed Aden Nur, ambaye anashutumiwa kuwa
aliwasaidia Wamarekani kumuua kiongozi wa kundi hilo Ahmed Godane.
Mwingine
aliyepigwa risasi anadaiwa kuwa alisaidia Wamarekani kumuua Adnan
Garaar, anayeaminika kuongoza shambulio la kigaidi katika duka la
Westgate nchini Kenya mwaka wa 2013
Habari kubwa Magazetini Kenya leo January 9, 2024
-
Good Morning Mtu wangu wa nguvu kutoka Tanzania January 9,
2024,nakukaribisha kutazama kile kilichoandikwa katika kurasa za mbele na
za nyuma Magazetini ...
5 hours ago