Recent Posts

PropellerAds

Saturday, June 4, 2016

Atletico Madrid yatinga fainali ligi ya mabingwa

Griezmann
Klabu ya soka ya Atletico Madrid imefanikiwa kutinga fainali ya klabu bingwa barani Ulaya kwa mara ya pili ndani ya kipindi cha miaka mitatu baada ya kupata bao la ugenini walipokipiga dhidi ya Bayern Munich ya Ujerumani.
Atletico wakiwa na faida ya bao la nyumbani katika nusu fainali ya kwanza nchini Uhispania, Bayern walisawazisha kupitia mkwaju wa adhabu ndogo uliopigwa na Xabi Alonso kwenye mechi ya Jumanne iliyochezewa uwanja wao wa nyumbani wa Allianz Arena.
Mlinda mlango wa Atletico Jan Oblak aliokoa mkwaju wa penalti uliopigwa na Thomas Muller kabla ya mshambuliaji Antoine Griezmann kusawazisha na kuwa 1-1.Madrid
Robert Lewandowski alifunga bao la pili baada ya kupokea pasi ya mpira wa kichwa kutoka kwa Arturo Vidal huku Atletico wakishindwa kusawazisha baada ya mkwaju wa penalti uliopigwa na Fernando Torres kuokolewa na mlinda mlango Manuel Neuer.
Matokeo ya jumla ya nusufainali hiyo yalimalizika sare 2-2 lakini Madrid wakasonga kwa kuwa na bao la ugenini.
Sasa Atletico watakutana na mshindi wa mchezo kati ya Real Madrid na Manchester City utakaopigwa kesho dimbani Santiago Bernabeu katika fainali mjini Milan tarehe 28 Mei.

www.facebook.com

Related Posts:

  • Korea Kaskazini yarusha kombora jingine Maafisa wa kijeshi nchini Korea Kusini wanasema Korea Kaskazini imejaribu kurusha kombora kutoka kwa manowari ya kivita na kukiuka vikwazo vya kimataifa Wanasema kuwa kombora hilo hatahivyo lilifeli muda mfupi baada ya ku… Read More
  • "Everybody has a wheelchair" Bert Burns understands God has a plan for our lives By Duane Cross We are hard pressed on every side, but not crushed; perplexed, but not in despair; persecuted, but not abandoned; struck down, but not destroyed. — 2 Cori… Read More
  • Mamia kupigwa picha za utupu Uingereza Mamia ya watu watavua nguo zao na kupigwa picha wakiwa tupu kusherehekea utamaduni katika mji wa Hull, Uingereza. Tukio hilo litakuwa la kusherehekea mji huo kama Mji wa Utamaduni. Washiriki watapakwa rangi ya samawati Jum… Read More
  • Sudan Kusini:Idadi ya waliouawa haijulikani Ripoti kutoka mji mkuu wa Sudan Kusini Juba ,zinasema kuwa mili mingi imepelekwa katika hospitali kuu ya mji huo baada ya ufyatulianaji mkali wa risasi kuibuka karibu na nyumba ya rais siku ya Ijumaa. Idadi ya watu walio… Read More
  • Moise Katumbi: Serikali ya DRC ilijaribu kuniuaKiongozi wa upinzani nchini DRC ambaye pia ni mgombea wa kiti cha urais katika uchaguzi ujao amesema kuwa serikali ya rais Joseph kabila ilimpa sumu katika njama ya kumuua. Mwanasiasa Moise Katumbi wa Jamhuri ya kidemokrasia … Read More