Israel na Uturuki wanatarajiwa leo kutia sahihi
mapatano yanayonuia kumaliza uhasama kati ya
mataifa hayo mawili.
Uhusiano wa karibu baina ya mataifa hayo uliharibika
miaka sita iliyopita wakati wanamaji wa Israeli
waliposhambulia meli ya Wanaharakati wa Uturuki
waliokuwa wakipeleka msaada wa vyakula na madawa
huko Palestina kwenye ukingo wa Gaza na kuwaua 10
kati yao.
Maafisa kutoka mataifa hayo mawili wanasema kuwa
mapatano yameafikiwa kumaliza uhasama huo.
Uhusiano umeimarika tangu Waziri Mkuu wa Israil,
Benjamin Netanyahu na mwenzake wa Uturuki Recep
Tayyip kuwasiliana kwa simu mwaka wa 2013, kabla ya
mashauriano kuanza na yameimarika kwa miezi
michache iliyopita.
Miongoni mwa hatua za kwanza itakuwa kuwarudisha
mabalozi wa mataifa hayo waliorejeshwa nyumbani
baada ya meli ya wakereketwa wa Uturuki waliokuwa
wakisafirisha chakula kuwapelekea Wapalestina
kushambuliwa na Israel.
Aidha baadhi ya mapendekezo ni Israeli kuomba
msamaha kwa uturuki na kisha kufidia wanaharakati
waliouawa.
Tanzania mwenyeji mkutano 63 wa baraza la Kimataifa la viwanja vya ndege
Afrika
-
Tanzania imeteuliwa kuwa mwenyeji wa Mkutano wa 73 wa Baraza la Kimataifa
la Viwanja vya Ndege (Airports Council Interantional-ACI) kwa Kanda ya
Afrika,h...
23 minutes ago