Roboti hiyo itakuwa ya kwanza kuhudumu katika jumba la matibabu baada ya roboti nyengine kuwekwa katika maduka ya uuzaji bidhaa, benki na vituo vya treni.
Hospitali moja inamipango ya kuajiri roboti zaidi kwa miaka 10 ijayo.
Baadhi ya wataalamu wamehoji umuhimu wa roboti za kijamii kama vile Pepper.
Kampuni ya softbank, iliyomtengeneza Pepper na kampuni ya Aldebaran wamepata faida kubwa kwa ubunifu huyo haswa kutoka Japan.
Roboti hiyo inaurefu wa kina futi nne na inauwezo wa kutambua sauti za binadamu kwa lugha 20 na inauwezo wa kubaini iwapo inazungumza na mwanamume, mwanamke au mtoto.