Recent Posts

PropellerAds

Monday, June 13, 2016

Uzito mkubwa hatari kwa utapia mlo

Utafiti mpya umeonya juu ya ongezeko la uzito mkubwa wa watu duniani ambao unaweza kusababisa kusambaa kwa kasi kwa utapia mlo.
Kwa kawaida,utapiamlo unaweza kuhusishwa na njaa. Lakini katika ripoti hii ya utapiamlo kimataifa ya mwaka huu, inaonesha kuwa watu walio na uzito mkubwa umeathiri mamilioni ya watu pia na kusababisha utapia mlo.
Watu hao utafiti umebaini kuwa wanatumia sukari kwa kiwango kikubwa,chumvi au mafuta katika damu zao na hawapati lishe bora.
Ripoti hiyo imeonya pia juu ya suala la afya kwa ujumla na maendeleo,na kutaka rasilimali zaidi kuwekezwa ili kuweza kukabiliana na tatizo hilo ambalo linaweza kuleta athari kwa muda mrefu.