
Mji wa Hong Kong ndio mji ghali
zaidi duniani baada ya kuupiku mji wa Luanda, Angola kulingana na
wafanyakazi wa kimataifa katika utafiti wa kila mwaka unaofanywa na
shirika la Mercer.
Luanda ambao ulikuwa unaongoza orodha hiyo katika siku za hivi karibuni ulishuka kufuatia kudhoofika kwa sarufi yake.
Mji wa Zurich na Singapore ni ya tatu na nne mtawalia katika orodha hiyo ikiwa haijabadilika kwa mwaka mmoja sasa.
Mji wa Tokyo sasa umepanda hadi nafasi ya tano.

