Rais wa Senegal Macky Sall, ametoa ilani ya kumsamehe waziri wa zamani nchini humo, Karim Wade kwa makosa ya ufisadi.
Karim
Wade, mpinzani mkubwa wa Rais Sall na mwanawe aliyekuwa Rais wa nchi
hiyo Abdoulaye Wade, hapo mwaka jana alihukumiwa jela kifungo cha miaka
sita.Kwa mjibu wa amri hiyo iliyotiwa saini mapema leo Ijumaa, Karim Wade na washtakiwa wengine wawili sasa wako huru, lakini ni sharti alipe fedha zinazodaiwa ziliibwa katika kashfa kubwa ya ufisadi.
Kuna taarifa kuwa Bwana Wade tayari ameondoka Senegal, kuelekea Ufaransa au Qatar.