Mawakili wa FIFA wasema washukiwa
wakuu wa madai ya ufisadi ambao hadi hivi majuzi walikuwa wakiliongoza
shirikisho hilo la kandanda duniani walijilimbikizia nyongeza za
mishahara na marupurupu mengineyo ambayo yamejumuishwa na kufika dola
millioni 80.
FIFA imeelezea kuwa malipo hayo yaliodhinishwa katika
kipindi cha miaka mitano na kupewa miongoni mwao Sepp Blatter, Jerome
Valcke na Markus Kattner si halali kwa mujibu wa sheria za Uswizi.Ushahidi unaokusanywa utakabidhiwa waendesha mashtaka wa Marekani na Uswizi
FIFA imeyafichua hayo baada ya polisi wa Uswizi kufanya uvamizi katika ofisi zilizoko makao makuu ya Zurich nchini Uswizi.
Tayari akina Blatter na Valcke wameshafunguliwa mashtaka mengine ya matumizi mabaya ya fedha za FIFA madai wanayokana.