Recent Posts

PropellerAds

Thursday, June 9, 2016

Muhammad Ali aombolezwa


Maelfu ya watu wamehudhuria swala ya kiislamu ya kumuombea aliyekuwa mwandondi bingwa duniani Muhammad Ali -- ambae alikufa wiki iliyopita.
Swala hiyo imefanyika katika ukumbi wa 'Freedom Hall' katika mji aliokulia wa Louisville.Waombolezaji walisikika wakimpa sifa Muhammad Ali kwa kuulita jina lake wakati mwili wa bondia huyo ulipoingizwa ukumbini.
Viongozi wakubwa katika ulimwengu wa ndondi na wanaharakati walikuwa sehemu ya waliohudhuria.Swala imeongozwa na Imam wa California, sheikh Zaid Shakir, ambae alikuwa pembezoni mwa Muhammad Ali pindi alipokuwa anakata roho na kupata fursa ya kumwombea dua ya mwisho kabla ya maziko.
Itakumbukwa kuwa, ukumbi wa Freedom Hall ndio sehemu ambayo pambano la mwisho la Muhammad Ali lilifanyika.Wakati huo huo , serkali ya kongo kinshasa imepanga kufanya sherehe rasmi ya kumkumbuka mwanandodi huyu ambae alipambana dhidi GEROGES FOREMAN mwaka 1974, inchini humo kwa mwaliko wa aliyekuwa rais wa nchi hiyo Mobutu Seseko.

Related Posts:

  • Mwanamke wa Senegal ateuliwa katibu mkuu Fifa Kwa mara ya kwanza katika historia, mwanamke ameteuliwa kuwa katibu mkuu wa Shirikisho la Soka Duniani (FIFA), shirikisho ambalo kwa kiwango kikubwa limetawaliwa na wanaume. Bi Fatma Samba Diouf Samoura kutoka Senegal, nd… Read More
  • Korea Kaskazini 'inaihami DR Congo'Ripoti ya siri ya wataalamu wa Umoja wa mataifa ilioonekana a shirika la habari la Reuters inaarifu kuwa maafisa kadhaa katika Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo wamesema kuwa Korea kasakzini imewapatia wanajeshi na polisi ba… Read More
  • Papa aruhusu mjadala wa wanawake mashemasiPapa aliahidi kubuni tume kutafiti na kujadili uwezekano huo wa kuwezesha wanawake kuhudumu katika ngazi hiyo ambayo ni daraja moja tu chini ya makasisi. Wanahistoria wanasema zamani wanawake walihudumu kama mashemasi. M… Read More
  • Twitter ya mtumbua jipu Mwanamuziki Mwanamuziki wa mtindo wa Rap Azealia Banks amepigwa marufuku na mtandao wa Twitter. Nyota huyo wa 212 amezuiliwa kuingia katika mtandao huo kufuatia hatua yake ya kutumia mtandao huo kumtusi msanii Zayn Malik. Ameshtumiwa k… Read More
  • Mwanamke mkongwe zaidi duniani afariki New York Mwanamke aliyetambuliwa kuwa mkongwe zaidi duniani ameaga dunia akitibiwa jijini New York, Marekani, madaktari wamesema. Susannah Mushatt Jones, amefariki akiwa na umri wa miaka 116 Alizaliwa eneo la mashambani jimbo la Al… Read More