Mgombea wa kiti cha urais wa chama
cha Republican nchini Marekani Donald Trump, amesema mauaji ya watu 50
katika baa moja ya wapenzi wa jinsia moja huko Orlando inathibitisha
msimamo wake kwamba waislamu wapigwe marufuku kukanyaga ardhi ya
Marekani.
Trump amemkashifu mpinzani wake wa chama cha republican
Bi Hillary Clinton, kwa kutodadisi sababu za mtu huyo kutenda mauaji
hayo.Babake Mateen amesema anaamini kitendo alichokifanya wanawe kilitokana na msukumo wa hisia zake dhidi ya wanaondeleza mapenzi ya jinsia moja na wala si kwa sababu za kidini.
Naye mkewe wa zamani Sitora Yusufiy, amemwelezea Mateen kama mtu wa aliyekuwa tabia za kigomvi na kutaka kupiga watu lakini hakuwa na itikadi kali za kidini.