Recent Posts

PropellerAds

Sunday, May 8, 2016

34 waangamia katika mafuriko Rwanda


Watu wasiopungua 34 wameaga dunia nchini Rwanda kufwatia mafuriko makubwa katika maeneo ya kaskazini mwa nchi hiyo.
Kulingana na mwandishi wa BBC nchini humo, barabara inayounganisha mji mkuu Kigali na miji ya Musanze na Rubavu Kaskazini Magharibi mwa Rwanda imekuwa haipitiki.
Vilima vilivyoko eno hilo vimeporomoka na kufunika barabara hiyo.
Hasara iliyopatikana kufwatia mafuriko hayo ni kubwa kwa mujibu wa naibu mkuu wa wilaya ya Gakenke ambayo imeathiriwa sana na mafuriko hayo .
Kiongozi huyo Bi Catherine Uwimana amesema
“Mvua kubwa ilinyesha tangu Jumamosi na kusababisha maporomoko makubwa ya ardhi ambayo hadi sasa watu 34 wamefariki dunia.
''Watu 19 waliojeruhiwa wamelazwa katika hospitali na zahanati za eneo hilo.
''Nyumba zaidi ya 400 zimeharibika kabisa huku miundo mbinu kama madaraja,barabara zinazounganisha kata,waya wa umeme, simu na mkonga wa mawasiliano yaani kila kitu kimesombwa na maji.”
Bi Uwimana ameonya kuwa kuna hofu ya maafa zaidi kwa sababu mvua bado inaendelea kunyesha kwa wingi katika eneo hilo.

Related Posts:

  • Atletico Madrid yatinga fainali ligi ya mabingwa Klabu ya soka ya Atletico Madrid imefanikiwa kutinga fainali ya klabu bingwa barani Ulaya kwa mara ya pili ndani ya kipindi cha miaka mitatu baada ya kupata bao la ugenini walipokipiga dhidi ya Bayern Munich ya Ujerumani… Read More
  • Thoughts for the Next Generation of Leaders  Last week Athletes in Action launched a NextGen Leadership initiative. Nearly two years in the planning, we had 19 staff members and 19 coaches from the business world taking part. It was a spectacular launch to th… Read More
  • Serikali ya Kenya yasema shisha ina Cocaine Wizara ya afya ya Kenya imekuwa ikitoa tahadhari dhidi ya matumizi ya uvutaji wa shisha ,katika siku hii ya kuadhimisha siku ya tumbaku duniani. Siku hii ilitengwa na Shirika la Afya duniani kuwaonya watu kuhusu hatari za… Read More
  • Waliokuwa maafisa wa Fifa walijipatia $80m Mawakili wa FIFA wasema washukiwa wakuu wa madai ya ufisadi ambao hadi hivi majuzi walikuwa wakiliongoza shirikisho hilo la kandanda duniani walijilimbikizia nyongeza za mishahara na marupurupu mengineyo ambayo yamejumui… Read More
  • Bondia Muhammad Ali alazwa hospitalini Bingwa wa dunia wa uzani wa juu wa zamani Muhammad Ali amelazwa hospitalini kufuatia maambikizi ya mapafu. Bondia huyo nyota mwenye umri wa miaka 74 aliyekonga nyoyo za wapenzi wa ndondi kote duniani anasemekana kuwa kati… Read More