Recent Posts

PropellerAds

Friday, May 27, 2016

Rais Obama atembelea mji wa Hiroshima

Rais Barrack Obama amekuwa rais wa kwanza aliye
mamlakani nchini Marekani kutembelea mji wa
Hiroshima tangu shambulio la nuklia wakati wa vita
vya pili vya dunia.
Obama amesema kuwa kumbukumbu za tarehe 6
mwezi Agosti 1945 hazifai kusahaulika,lakini hakuomba
msamaha wa shambulio hilo la Marekani ikiwa ni bomu
la kwanza la kinyuklia kutumika duniani.
Bw Obama alizungumza na baadhi ya walionusurika na
katika hotuba yake akayataka mataifa kujiendeleza bila
silaha za kinuklia.
Takriban watu 140,000 walifariki mjini Hiroshima na
wengine 74,000 siku mbili baadaye katika bomu la pili
katika mji wa Nagasaki.
Bw Obama alitembelea makavazi ya Heroshima kabla
ya kuelekea katika eneo la kuhifadhi kumbukumbu za
shambulio hilo,akiandamana na waziri mkuu Shinzo
Abe.Wote wawili walisimama mbele ya mwanga wa
milele.