Takriban watu 50 wamefariki kufautia mafuriko na maporomoko ya
ardhi yaliosababishwa na mvua kubwa katika baadhi ya maeneo Ethiopia.
Taifa
hilo la upembe wa Afrika linakabiliwana ukame mbaya kuwahi kushuhudiwa
katika miaka 50 huku watu zaidi ya milioni 10 wakiwa wanahitaji msaada
wa dharura wa kibinaadamu.
Ukame huo umezidhishwa kuwa mbaya kutokana mvua ya El Nino inayoaathiri baadhi ya mataifa Afrika mashariki na kusini.
Maafisa
wa serikali katika wilaya iliopo kusini mwa Ethiopia Wolaita
wamekiambia kituo cha televisheni ya serikali kuwa watu 41 waliuawa
Jumatatu katika maporomoko ya ardhi yaliotokana na mvua kubwa
inayoendelea kunyesha nchini.
Wengine 9 walifariki kuisni mashriki mwa eneo la Bol ambako mamia ya mifugo pia ilizama.
Maelfu ya watu pia wamepoteza makaazi yao, walisema maafisa.
Mafuriko yametatiza jitihada za kuwaisaidia watu wanaohitaji usaidizi baada ya barabara nyingi na vivukio kuharibika kabisa.
Serikali
na mashirika yamisaada yameanzisha ombi la msaada wa thamani ya dola
bilioni 1.4 kuwasiaidia mamilioni ya watu wanaohitaji kwa dharura
chakula.
Anayedaiwa kumchoma moto mwanamke katika njia ya treni kufikishwa mahakamani
-
Mwanamume anayedaiwa kumchoma moto mwanamke aliyekuwa amelala hadi kufa
ndani ya treni ya chini ya ardhi ya Jiji la New York anatarajiwa kufikishwa
mahak...
15 hours ago