Aliyekuwa mgombea wa urais wa tiketi ya chama cha
Republican nchini Marekani, Jeb Bush, amesema kuwa
hatampigia kura Donald Trump katika Uchaguzi wa
Novemba.
Bwana Bush alisema kuwa Trump hana tabia wala
mienendo ya kuwa Rais wa Marekani.
Jeb ni mojawapo wa wanachama mashuhuri wa
Republican kutanganza hadharani kuwa hatompigia
kura Bwana Trump kwa sababu ya kampeni yake ya
kiburi ambayo imegawanya chama cha Republican.
Mnamo Alhamisi Spika wa Bunge, Paul Ryan, alisema
kuwa hatamuunga mkono mfanyabiashara huyo tajiri,
ingawa atakutana naye juma lijalo.
Hata hivyo Bwana Trump ameungwa mkono na
mgombezi wa Urais wa zamani Bob Dole aliyeshindwa
katika uchaguzi na Bill Clinton wa chama cha
Democratic mwaka 1996.
Habari kubwa Magazetini Kenya leo January 10, 2024
-
Good Morning Mtu wangu wa nguvu kutoka Tanzania January 10,
2024,nakukaribisha kutazama kile kilichoandikwa katika kurasa za mbele na
za nyuma Magazetini...
4 hours ago