Aina moja ya almasi ya rangi ya
waridi imeuzwa pesa nyingi zaidi katika historia, ambazo ni dola milioni
31.5 kwenye mnada mjini Geneva.
Almasi hiyo yenye carat 15.38
ilipatikana nchini Afrika Kusini chini ya miaka mitano iliyopita, kwa
mujibu wa shirika la habari la AFP.Ilipachikwa kwenye pete na kuuzwa kwa mfanyi biashara mmoja kutoka Asia, ambaye aliinunua kwa kuwasiliana kwa njia ya simu.
Hiyo ndiyo bei ya juu zaidi kuwai kulipwa kwa almasi ya rangi ya waridi.