Recent Posts

PropellerAds

Tuesday, May 10, 2016

Polisi waandamana dhidi ya Beyonce


Kundi moja la maafisa wa polisi limefanya maandamano karibu na tamasha lililofanyika katika mji wa nyumbani wa nyota wa muziki Beyonce huko Houston.
Wanachama wa muungano wa polisi na Sherrif walisimama mbali na uwanja wa soka na kuelekeza mwangaza wa bluu katika ukumbi wa tamasha hilo.
Walikuwa wanapinga kanda ya video ya Beyonce ambayo wanasema inawaponza polisi.

Mwanamuziki huyo tayari amesema kwamba hawakosoi polisi katika wimbo huo na kusema kuwa maafisa wa polisi wanaodhani aliwaponza wanakosea.
Mwanachama mmoja wa polisi amekiambia chombo cha habari KHOU11 kwamba hawakufurahia baada ya Beyonce kutumia picha za gari moja la polisi mjini New Orleans iliokuwa ikizama katikamafuriko.
''Tunaamini kwamba baadhi ya mambo yake ni kinyume na maafisa wa polisi'',alisema.

Mnamo mwezi Aprili,Beyonce aliambia jarida la Elle kwamba anaheshimu polisi lakini hapendi unyanyasaji.
''Mtu yoyote anyedhani kwamba siwapendi polisi anakosa kwa sababu'', alisema.
''Ninawapenda na kuwaheshimu sana polisi pamoja na familia za maafisa hao ambao hujitolea ili kuhakikisha tuko salama''.

Related Posts:

  • MAGAZETI YA LEO TZ,MARCH 29 Read More
  • Aliyesaidia El Chapo kulangua pesa anaswaMaafisa wa usalama nchini Mexico wamemkamata mwanamume wanayesema alisaidia kulangua pesa kwa niaba ya mlanguzi wa mihadarati Joaquin Guzman, aliyejulikana sana kama "El Chapo" au "Shorty". Juan Manuel Alvarez Inzunza, kwa ji… Read More
  • Marekani yalalamikia UN kuhusu IranMarekani na washirika wake kutoka Ulaya wameulalamikia Umoja wa Mataifa kuhusu hatua ya Iran ya kufanyia majaribio makombora ya masafa marefu. Mataifa hayo yamesema majaribio hayo yanakiuka azimio la Umoja wa Mataifa. Azimio … Read More
  • Sharif aahidi kuangamiza magaidi PakistanWaziri Mkuu wa Pakistan Nawaz Sharif ametoa wito kwa kuwepo ushirikiano zaidi kati ya idara za usalama nchini humo ili kukabiliana na ugaidi. Amesema hayo siku moja baada ya watu zaidi ya 70 kuuawa kwenye shambulio la bomu ka… Read More
  • 'Al-Shabab 100 wauawa' vitani SomaliaKiongozi wa jimbo la Galmudug, katikati mwa Somalia amesema wanajeshi wa jimbo hilo wamewaua zaidi ya wapiganaji 100 wa al-Shabab kwenye mapigano yaliyodumu siku nne. Wapiganaji hao wa Kiislamu walikuwa wameingia jimbo hilo w… Read More