Maafisa wawili wa Trafiki wameuawa katika mlipuko wa kujitoa
muhanga wa gari, uliotokea katika makao makuu ya idara ya trafiki mjini
Mogadishu.
Milipuko mikubwa ilisikika katika makao hayo makuu ya Trafiki huko Shangani Mogadishu, na baadaye kufuatia na ufyetuaji risasi.
Wapiganaji wa kundi la al-Shabab wamedai kuhusika.
Katika taarifa yao kundi hilo limedai kwamba shambulio hilo lilipangwa vyema.
Mpiganaji
mmoja aliliendesha gari lililokuwa na vilipuzi na mwingine alijaribu
kuyavamia makao hayo makuu ya trafiki, lakini alipigwa risasi, Abdifatah
Omar Halane, msemaji wa utawala wa mj wa Mogadishu ameliambia AFP.
Mara nyingi Al-Shabab hushambulia maeneo ya jeshi na raia katika kampeni yake ya kuipindua serikali ya Somalia.
Anayedaiwa kumchoma moto mwanamke katika njia ya treni kufikishwa mahakamani
-
Mwanamume anayedaiwa kumchoma moto mwanamke aliyekuwa amelala hadi kufa
ndani ya treni ya chini ya ardhi ya Jiji la New York anatarajiwa kufikishwa
mahak...
15 hours ago