Jiji la London limemchagua Meya wa kwanza
Muislamu, Sadiq Khan, aliyekuwa wakati mmoja Waziri
katika chama cha upinzani cha Laba.
Bwana Khan ni mwana wa dereva wa zamani wa bas
jijini London aliyezaliwa Pakistan. Alipata kura milioni
moja na mia tatu elfu.
Hicho ni kiwango kikubwa sana cha kura kuwahi
kupigiwa Meya ye yote jijini London.
Katika hotuba yake ya ushindi, Bwana Khan aliahidi
kuongoza kwa niaba ya wakaazi wote wa London.
Wasimamizi wa kampeni ya mpinzani wake katika
uchaguzi huo Zac Goldsmith, ambaye ni tajiri mkubwa
walishutumiwa kwa kudai kuwa Bwana Khan ana
uhusiano na Waislamu wenye itikadi kali.
Bwana Khan alisema kuwa wakaazi wa London
wamepiga kura ya umoja na kuponza mgawanyiko.
Ushindi huo ni wa kumtia moyo kiongozi wa chama cha
Labour Jeremy Corbyn.
Chama chake kilipata ushindi dhaifu katika maeneo
mengine ya nchi katika uchaguzi huo.
Habari kubwa za Magazeti ya Tanzania leo January 10, 2024
-
Good Morning Mtu wangu wa nguvu kutoka Dar es salaam January 10,
2025,nakukaribisha kutazama kile kilichoandikwa katika kurasa za mbele na
za nyuma za Ma...
59 minutes ago