Yoweri Museveni leo ametawazwa rasmi kuwa Rais
mpya wa Uganda kwa muhula wa tano mfululizo.Tayari
Rais Museveni amekwisha tawala miaka 30.
Kutawazwa kwake leo, ambako kunashuhudiwa na
viongozi wa mataifa 14 kutoka Afrika na wageni
wengine mashuhuri, kuna fuata ushindi uliojaa
ubishani katika uchaguzi wa Februari 18.
14.18pm: Katika ufisadi Museveni amesema kuwa
kucheleweshwa kuchukuliwa kwa hatua kunawaudhi
raia na kutowavutia wawekezaji
14.16pm: Amesema kuwa Uganda imekuwa na amani
kwa mara ya kwanza katika kipindi cha miaka
500.''Hakuna mtu anayeweza kuharibu usalama wa
Uganda''.Amewataka wenzake wa Afrika kuimarisha
usalama wa Somalia na Congo
14.11pm: Amewataka wakulima kulima kahawana
chai.Amesema kila nyumba lazima ishiriki katika kilimo.
13.57pm: Museveni-Uchumi wetu umekuwa sana lakini
tatizo ni kwamba tunanunua vitu vingi kutoka nje na
tunauza vichache.
Amewapongeza raia wa Uganda kwa kupiga kura kwa
wingi katika kila sekta ya uongozi.Vilevle amevipongeza
vyama vya upinzani kwa kushinda viti mbali mbali.
13.45pm: Rais wa Deby amehutubia kwa lugha ya
kifaransa.
13.33pm: Museveni asema ICC ni bodi isiyo na
maana.''Tuliunga mkono icc tukidhani ni mahakama
nzuri lakini baadaye tukagundua ni mahakama yenye
watu wasio na maana''.Museveni ameyasema hayo
baada ya kumtambua rais wa Sudan Omar el Bashir
13.23pm: Baadhi ya viongozi waliotambuliwa katika
sherhe hiyo ni rais Uhuru Kenyatta wa kenya
Yoweri museveni amkaribisha rais wa Zimbabwe,Omar
el bashir wa Sudan.
13.17pm: Miongoni mwa marais wanaohudhuria sherehe
hiyo ni pamoja na rais wa Sudan Omar el Bashir
anayeswaka na mahakama ya uhailifu wa kivita katika
eneo la Darfur na rais wa Afrika Kusini Jacob Zuma .
13.13pm: Jeshi la Uhanda latoa heshima zao kwa rais
Museveni hivi sasa.
13.09pm: Wimbo wa taifa unaimbwa
12.56pm: Ni wakati ambapo ndege za jeshi zinatoa
heshima zao kwa rais Museveni.Ndege hizo
zinaonyesha uwezo wake wa kulilinda taifa la Uganda
chini ya uongozi wa rais Museveni.
12.38pm: Museveni amekabidhiwa vifaa muhimu vya
madaraka ikiwemo katiba,ngao ya mamlaka,bendera na
upanga ambao ni ishara ya jeshi.
Na sasa ni zamu ya jeshi la taifa hilo kumpatia heshima
rais huyo.
12.15pm :Rais Museveni alikagua gwaride la jeshi baada
ya kuapishwa rasmi
12.10pm: Rais Yoweri Museveni aapishwa rasmi na jaji
mkuu
12.05pm: leo rasmi imetangazwa kuwa siku ya
mapumziko ili watu watokeze kwa wingi kwa sherehe
hizo. Ingawaje bado kuna hali ya wasiwasi kwa vile
chama cha upinzani na FDC na mgombea urais wa
zamani Dk Kizza Besigye bado wanakana ushindi wa
Museveni.
12.00pm: Rais Yoweri Museveni kuapishwa kuwa rais
kwa muhula wa saba mfululizo nchini Uganda
Museveni kumkabidhi madaraka Museveni si jipya kwa
Waganda. nani Rais ambaye alilaumu mwaka 1986,
viongozi wa Afrika kukaa madarakani kwa muda mrefu
sana.
Anayedaiwa kumchoma moto mwanamke katika njia ya treni kufikishwa mahakamani
-
Mwanamume anayedaiwa kumchoma moto mwanamke aliyekuwa amelala hadi kufa
ndani ya treni ya chini ya ardhi ya Jiji la New York anatarajiwa kufikishwa
mahak...
16 hours ago