Recent Posts

PropellerAds

Wednesday, May 18, 2016

Trump: Ninaweza kuzungumza na Kim Jong-un

Marekani
Mgombea urais wa chama cha Republican nchini Marekani Donald Trump amesema yuko tayari kufanya mazungumzo na kiongozi wa Korea Kaskazini kuhusu mpango wa nyuklia wa taifa hilo.
“Ninaweza nikazungumza naye, Siwezi kuwa na tatizo kuzungumza naye,” Bw Trump alisema kuhusu Kim Jong-un.
Mkutano huo ungekuwa tofauti kabisa na msimamo wa muda mrefu wa Marekani kuhusu Korea Kaskazini.
Hatua hiyo imemfanya mgombea anayeongoza katika kinyang’anyiro cha chama cha Democratic Hillary Clinton kumshutumu Bw Trump na kusema anashangaza kwa kuwaenzi sana viongozi wababe wan chi za nje.
Taarifa iliyotolewa na mmoja wa wasaidizi wa Bi Clinton imesema sera ya mambo ya nje ya Bw Trump usio wa maana yoyote.
Kwingineko, BBC imefahamu kwamba huenda Bw Trump akazuru Uingereza kabla ya kufanyika kwa uchaguzi mkuu nchini Marekani mwezi Novemba.
Wanadiplomasia wanatarajia ziara hiyo ifanyike baada yake kuwa rasmi mgombea urais wa chama cha Republican mwezi Julai.
Mapema wiki hii, Bw Trump alisema dalili zinaonesha huenda asiwe na uhusiano mwema sana na Uingereza.
Waziri Mkuu wa Uingereza David Cameron na meya mpya wa London Sadiq Khan, ambaye ni Mwislamu, wamemshutumu Bw Trump kutokana na hatua yake ya kupendekeza Waislamu wazuiwe kuingia Marekani.