Uhaba mkubwa wa mafuta umeshuhudiwa katika mji mkuu wa Bujumbura na maeneo mengine nchini Burundi.
Kwa
karibu wiki moja sasa, vituo vya kuuza mafuta vimekabiliwa na uhaba
mkubwa na wateja wanalazimika kupanga foleni kwenye vituo ambavyo bado
havijamaliza mafuta.Waziri wa nishati nchini humo aliambia runginga ya taifa Alhamisi kwamba hakuna sababu yoyote ya kuvifanya vituo vya mafuta kukosa mafuta ya kuuaza.
Alisema taifa hilo bado lina mafuta ya kutosheleza mahitaji.
Mwandishi wa BBC aliyeko Bujumbura Prime Ndikumagenge anasema licha ya hakikisho la waziri, uhaba bado umeendelea kushuhudiwa.
Baadhi ya watu wanasema huenda wanunuzi wa mafuta kwa wingi wameshindwa kupata fedha za kigeni za kutosha kuagiza petroli kutoka nje.