Korea Kaskazini imesema kuwa itatumia silaha zake
za nyukilia kujilinda rais Kim Jong-unamesema.
Kiongozi wa wa taifa hilo lenye usiri mkubwa Kim Jong-
un aliwaelezea wajumbe wa kamati kuu ya chama
tawala Workers' Party mjini Pyongyang kuwa jeshi lao
litatumia silaha hizo za kitonoradi kulinda uhuru wa
taifa hilo utakapotishiwa.
Aidha rais Kim jong un aliwaeleza wajumbe hao kuwa
Korea Kaskazini sasa itaanza kusemezana na mataifa
yaliyokuwa mahasidi wao hapo awali.
Vyombo vya habari vya taifa vimemnukuu kiongozi huyo
akiambia baraza Kuu la chama cha wafanyikazi
kinachotawala kuwa kunapaswa kuwepo mashauriano
zaidi na Korea Kusini ili kuimarisha uelewano na
kuaminiana.
Inadaiwa pia kuwa alisema kuwa serikali yake itafanya
kila juhudi kupunguza kuenea kwa silaha za kinyukilia
duniani ingawa taifa lake lilijiondoa katika chama cha
kupunguza ongezeko la zana za kinukilia duniani mwaka
2003.
Korea Kaskazini ilifanya jaribio la silaha yake ya
kinukilia miaka mitatu baadaye na kuna uvumi kuwa
inatarajia kufanya jaribio la tano ili kwenda sambamba
na mkutano wa baraza Kuu la Cchama tawala
unaondelea hivi sasa.
Mara kadhaa serikali ya Korea Kaskazini imetisha
kushambulia Marekani na Korea Kusini kwa mabomu ya
kinyukilia.
Anayedaiwa kumchoma moto mwanamke katika njia ya treni kufikishwa mahakamani
-
Mwanamume anayedaiwa kumchoma moto mwanamke aliyekuwa amelala hadi kufa
ndani ya treni ya chini ya ardhi ya Jiji la New York anatarajiwa kufikishwa
mahak...
15 hours ago