Recent Posts

PropellerAds

Friday, May 6, 2016

band ya muziki yamzingua Trump kucheza muziki wao


Wanamuziki wa The Rolling Stones wamemtaka mgombea wa urais kupitia tiketi ya chama cha Demokrat Donald Trump kuwacha kucheza muziki wao wakati wa kampeni zake za urais.
Bendi hyo imetoa taarifa ikisema kuwa mgombea huyo wa uraisi hana ruhusa ya kucheza nyimbo zao na wametaka asitishe kufajnya hivyo mara moja.
Bendi ya Rolling Stones haijatoa ruhusa kwa kampeni ya Trump kutumia nyimbo zao na sasa inaitaka kampeni hiyo kukoma kutumia muziki wake mara moja.
Mgombea huyo amekuwa akicheza nyimbo hizo katika mikutano yake ya kampeni kwa miezi kadhaa sasa.Kibao chao kilichovuma mwaka 1969 ''You Cant Always Get What You Want'' kimekuwa maarufu.
 
Bendi hiyo sio ya kwanza kutoa lalama kama hizo kwa nyota huyo wa runinga na mfanyibiashara.
Mnamo mwezi Februari ,Adele alitoa taarifa akijiondoa katika uhusiano wowote na Trump baada ya kucheza muziki wa nyota huyo ''In The Deep'' katika mikutano yake.
Mwanamuziki huyo alitoa taarifa akiweka wazi kwamba hajampatia ruhusa mgombea huyo kutumia muziki wake kwa kampeni zake za kisiasa

Related Posts:

  • Florentin Pogba kukabiliana na nduguye Paul PogbaMchezaji wa kimataifa wa Guinea Florentin Pogba amekiri kuwa mamake atakuwa katika hali ngumu wakati atakapotazama akimkabili nduguye mdogo Paul katika mechi ya ligi ya Europa. Siku ya Alhamisi Florentin ataichezea St Etienne… Read More
  • Kijana aponzwa na Adolf Hitler nchini Austria Polisi nchini Australia wametangaza kwamba imemkamata kijana mwenye umri wa miaka 25, ambaye alivalia mavazi yanayofanana na aliyewahi kuwa matawala wa manazi Adolf Hitler kwa makosa ya kuutukuza utawala na enzi ya wanaz… Read More
  • Watu zaidi wakamatwa kufuatia kifo cha Kim Jong-namWashukiwa wawili zaidi wamekamatwa kuhusiana na kifo cha Kim Jong-nam, ambaye ni ndugu wa kambo wa kiongozi wa Korea Kaskazini Kim Jong-un nchini Malaysia. Mshukiwa mmoja mwanamke raia wa Indonesia na mwanamume raia wa Malays… Read More
  • Baraza la makardinali lamshangaa Papa Baraza kuu la ushauri linaloongozwa na kiongozi mkuu wa kanisa katoliki ulimwenguni Papa Francis , limechukua hatua isiyokuwa ya kawaida ya kutoa taarifa yenye kuonesha kuwa linamuunga mkono. Hali hiyo inafuatia upinzan… Read More
  • Amuua mfanyakazi akidhani ni ngiri Afrika Kusini Watu nchini Afrika Kusini wamegadhabishwa, kufuatia taarifa za mwanamme mmoja, ambaye analaumiwa kwa kumuua kwa kumpiga risasi mfanyakazi wa shamba, akidhani kuwa mtu huyo ni ngiri. Stephen Hepburn alifikishwa mahakamani… Read More