DRCongo inatakiwa iarifu UN kuhusu ununuzi wowote wa silaha
Ripoti ya siri ya wataalamu wa Umoja wa Mataifa
ilioonekana a shirika la habari la Reuters inaarifu kuwa maafisa kadhaa
katika Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo wamesema kuwa Korea kazkasini
imewapatia wanajeshi na polisi bastola.
Wamesema pia Korea Kaskazini wamewatuma wakufunzi 30 kutoa mafunzo kwa kikosi cha ulinzi wa rais na vikosi maalum.
Marufuku iliyoidhinishwa dhidi ya Korea Kaskazini kuuza silaha inaizuia kununua, kuuza na pia kutoa mafunzo.
Na
marufuku dhidi ya Jamhuri ya kidemokrasi ya Congo inaihitaji nchi hiyo
kuiarifu kamati ya vikwazo katika baraza la usalama la Umoja wa mataifa
biashara yoyote ya kununua au kupokea mafunzo.
Wataalamu hao
wanasema wamegundua kuwa maafisa kadhaa wa jeshi la Congo pamoja na
maafisa wa polisi waiotumwa ng'ambo kama ujumbe wa Umoja wa Mataifa,
wanaonekana kuwa na bastola hizo za Korea Kaskazini.