Recent Posts

PropellerAds

Sunday, May 29, 2016

Makumbusho ya wanajeshi wa Ujerumani na Ufaransa yafanyika


Sherehe za miaka 100 za kuwakumbuka wanajeshi wa Ujerumani na Ufaransa waliouwawa wakati wa vita vikali vya muda mrefu enzi ya vita vikuu mwaka 1916 zinafanyika kaskazini mwa Ufaransa.
Sherehe hizo zilianza na hotuba kutoka kwa kansela wa Ujerumani Angela Merkel pamoja na mwenyeji wake wa Ufaransa, Francois Hollande.
 
Wote wawili waliweka shada za maua katika makaburi ya wanajeshi hao huko Consenvoye.
Zaidi ya wanajeshi laki tatu wa Ufaransa na Ujerumani waliuwawa katika makabiliano hayo, yaliyofanyika kaskazini mashariki mwa Ufaransa kwa zaidi ya miezi tisa mnamo mwaka 1916.